Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akifungua mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akisisitiza kuhusu namna idadi ya watu inavyoongezeka au kupungua wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Omary Mdoka akiwasilisha mada kuhusu ongezeko la watu wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Oscar Mangula akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya takwimu ya mwaka 2015 wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za kitakwimu Bw. Magnus Mahenge akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo Jijini Dodoma.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Mariam Kitembe akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi hapa nchini kwa kuzingatia utafiti uliofanyika mwaka 2016/2017 wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Said Ameir akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili.
Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Irenius Ruyobya akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu kwa waandishi wa habari wa Jiji la Dodoma leo.
(Picha zote na Frank Mvungi)