Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Habari
Jan 14, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39740" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mhandisi Hagai Mziray wa Mzinga Corporation kuhusu ramani ya jengo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara zinazojengwa na Kampuni ya Mzinga Corporation inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_39741" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na Watendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya Mzinga Corporation alipokuwa akifanya ukaguzi katika wa Ofisi zinazojengwa na Kampuni hiyo leo Ihumwa jijini Dodoma. Wizara zinazojengwa na Kampuni hiyo ni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michez, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Wizara ya Madini na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.[/caption] [caption id="attachment_39742" align="aligncenter" width="1000"] Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Lekumock Ponja akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi Sanifu wa Mzinga Corporation, Keneth Wambua kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_39743" align="aligncenter" width="1000"] Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Lekumock Ponja akitazama ujenzi wa jengo la Ofisi ya wizara hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_39749" align="aligncenter" width="1000"] Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Lekumock Ponja (kushoto) akitazama mchoro wa jengo la Ofisi ya wizara hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za wizara hiyo leo Ihumwa jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Katibu Muhtasi wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sana na Michezo, Bibi. Munieshi Mushi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara hiyo, Bi. Lorietha Laurence na Mhandisi Hagai Mziray wa Mzinga Corporation.[/caption] [caption id="attachment_39744" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya mafundi wa Kampuni ya ujenzi ya Mzinga Corporation wakiendelea na majukumu yao ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kama walivyokutwa leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_39746" align="aligncenter" width="1000"] Muonekano wa nje wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zinazojengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi