Matukio katika Picha: Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Jan 12, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya hesjima ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium jijini Zanzibar .
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Marium Mwinyi, (katikati) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, (kulia) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakisimama wakati wa kupokea salamu ya heshima ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kupokea salamu ya heshima ya Vikosi hivyo katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar
Vikundi mbalimbali vya maandamano vikipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
Kikosi cha Jeshi la KIKOSI CHA KUZUIA MAGENDO KMKM wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa haraka katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar
Baadhi ya Maofisa wa Vikosi vya Ulinzi na Wananchi wakifuatilia kwa karibu harakati za kusheherekea Maadhimisho ya Kilele cha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.