Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza kikao cha sita cha mkutano wa kumi na mbili cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe wakati wa kikao cha sita cha mkutano wa kumi na mbili Bungeni Jijini Dodoma.
Mwalimu Joyce Solomon wa Shule ya Tumaini Mission kutoka Arumeru akifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge pamoja na wanafunzi wa shule hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt Philip Mpango akisoma Muswada wa Sheria ya marekebisho ya sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi wa mwaka 2018 leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Mhandisi Isack Kamwelwe akitolea ufafanuzi juu ya changamoto za kivuko cha Mv Mafanikio katika kusaidia dharura zinazojitokeza kwa wagonjwa hasa akina mama wajawazito kuhudumiwa wakati wa usiku leo Bungeni Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Mhandisi Stella manyanya akielezea mipango mbalimbali ya Serikali katika kufanikisha azma nzuri ya uchumi wa Viwanda nchini leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akieleza mipango mbalimbali ya jeshi la kujenga Taifa katika kuanzisha mafunzo ya stadi za kazi kwa Vijana waliojiunga na jeshi ilo kwa kujitolea ili waweze kuajiriwa na taasisi zingine za Serikali,Sekta binafsi au kujiajiri wenyewe.