Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni leo 10 Aprili, 2018
Apr 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30093" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe ambapo alieleza mikakati ya serikali ya kuendelea kulinda na kuenzi tamaduni na maadili ya Mtanzania hasa katika sekta ya sanaa nchini, wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_30095" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akibalishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Ahmed Juma Ngwali, wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_30092" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo alisisitiza kuwa Serikali inayo vyombo vya kusimamia maudhui ya vyombo vya habari na matangazo, wakati wa mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.

[/caption] [caption id="attachment_30094" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Madini Mhe. Angela Kairuki (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi