Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kuna kiwango cha kutosha cha mafuta ya kula hapa nchini hasa kipindi hiki cha kuelekea msimu wa mfungo mtukufu wa Ramadhani mapema leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjwelwa akisisistiza jambo mapema leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjelina Mabula akieleza juu ya faida za hati za kimila ikiwemo kutumika kuwapatia mikopo wananchi ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akieleza mkakati wa Wizara yake kuhakikisha kuwa kila kijiji kinafikiwa na huduma ya umeme hapa nchini.
Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka akiuliza swali Bungeni kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha sekta ya viwanda katika mkoa wa Kagera, leo Bungeni Jijini Dodoma.