Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Matukio Katika Picha Bungeni Leo
Sep 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_13132" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasilisha azimio la Bunge kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda kuhusu mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) leo Bungeni mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.[/caption] [caption id="attachment_13133" align="aligncenter" width="900"] Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_13135" align="aligncenter" width="730"] Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akitoa maelezo kuhusu matumizi ya silaha za jadi hapa nchini na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia uzagaaji wa silaha hizo.[/caption] [caption id="attachment_13138" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Mhandisi Gerson Lwenge akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi katika Wilaya ya Ngara wanapata huduma za maji.[/caption] [caption id="attachment_13139" align="aligncenter" width="769"] Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia injinia Stella Manyanya akitoa ufafanuzi kuhusu jinsi Serikali ilivyofanikiwa katika mpango wa elimu bure hapa nchini.[/caption] [caption id="attachment_13140" align="aligncenter" width="720"] Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate Ole Nasha akizungumzia mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa Maafisa ugani katika maeneo yote hapa nchini wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuwahudumia wananchi.
(Picha na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma) P[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi