Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mashine za Kielektroniki Kuanza Kutumika Magogoni
Jun 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Lilian Lundo

Serikali inatarajia  kutoa huduma za ukatishaji wa tiketi kwa njia ya mfumo wa kielekroniki katika kivuko cha Magogoni ili kudhibiti mapato yanayopotea kiholela..

Akiongea na Maelezo jijini Dar es Saam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Dkt. Musa Mgwatu alisema kukamilika kwa mfumo huo utakaogharimu bilioni 1.1 kutasaidia kuiongezea mapato serikali kwani mfumo huo utafanyakazi kwa njia za kielekroniki.

“Ujenzi wa mashine za kielektroniki umeshaanza na kukamilika kwa upande wa magogoni, Mkandarasi anatarajia kuanza ufungaji wa mashine hizo upande wa Kigamboni wiki hii,” alifafanua Dkt. Mgwatu.

Dkt. Mgwatu alisema Mkandarasi wa mradi huo anatarajia kukamilisha uwekaji wa mashine hizo julai 25 mwaka huu na utumiaji wa mashine hizo utaanza kutumika tu mara baada ya makabidhiano kutoka kwa mkandarasi.

Akizungumzia gharama za kuvuka Dkt. Mgwatu amesema, gharama za kuvuka zitabaki pale pale na hakutakuwa na ongezeko lolote mashine hizo zitakapoanza kutumika.

Bwana Ismail Juma, mkazi wa Kigamboni amesema kuanzishwa kwa mfumo huo kumekuja wakati muafaka na kutasaidia kuiongezea mapato serikali na kuepusha upotevu wa mapato katika vivuko hivyo.

Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano  aliwaagiza TEMESA kufunga mfumo kamili wa kupokea nauli wa elektroniki ambao utadhibiti ukwepaji wa kulipa nauli ili kuongeza mapato.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi