Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mashindano ya Uandishi wa Insha Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira
Jun 04, 2020
Na Msemaji Mkuu

Tanzania itaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani tarehe 5 Juni, 2020. Katika maadhimisho ya mwaka huu, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau wa Mazingira imeandaa mashindano ya uandishi wa insha kuhusu masuala ya Mabadiliko ya tabianchi na mazingira.

Lengo ni kukuza uelewa na kuhamasisha ubunifu kwa wanafunzi na vijana katika masuala ya hifadhi ya mazingira pamoja na kubainisha uelewa wa kizazi cha sasa kuhusu sekta husika.

WALENGWA

Mashindano haya yanalenga kuhusisha wanafunzi katika ngazi ya shule za Msingi na Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini.

MADA

Shule za Msingi:

Athari za mabadiliko ya Tabianchi nchini

Shule za Sekondari: 

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye ustawi wa Bioanuai (Kidato cha 1 hadi 4)

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii (Kidato cha 5 hadi 6)

Vyuo Vikuu na vya Kati

Mikakati ya kitaifa na kimataifa ya kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

TATHMINI

Mawasilisho ya insha yatatathiminiwa kulingana na uhalisia na mifano ya maisha ya sasa, ubunifu na umahiri wa lugha iliyotumika katika maandiko (kingereza au kiswahili).

UREFU WA INSHA

  • Kwa Shule za Msingi, insha isizidi maneno mia tano (500)
  • Kwa Shule za Sekondari, insha isizidi maneno elfu moja (1000)
  • Kwa Vyuo vya Elimu ya Juu, Insha isizidi maneno elfu mbili (2000)

MUDA WA KUWASILISHA INSHA

Mwisho wa kupokea insha itakuwa tarehe 10 Juni, 2020.

Insha zitumwe kwa njia ya Email martha.ngalowera@vpo.go.tz au enock.sanga@vpo.go.tz watakaoandika kwa kalamu wascan karatasi husika na kutuma kwa njia ya email mojawapo iliyoainishwa hapo juu.

UTAMBULISHO

Muhusika aandike Jina kamili, shule/Chuo anachosoma, namba ya usajili wa shule /Chuo, Darasa/Kidato /mwaka wa chuo ambao muhusika yupo chuoni.

ZAWADI ZITAKAZOTOLEWA KWA WASHINDI ni pamoja na compyuta mpakato, Cheti cha ushindi, Begi na vifaa vya shule chupa ya kuwekea maji, na fulana na kofia. Kwa kila shule anayotoka mshindi watapata Mipira miwili pamoja na  vifaa vya kufundishia.

HAFLA YA KUTOA ZAWADI

Zawadi kwa washindi zitatolewa tarehe 17 Juni, 2020 siku ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani.

MAWASILIANO

Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana na Bw. Enock Sanga kupitia simu namba 0753 326 234 au Bi. Martha Ngalowera namba 0784589610. Pia tembelea tovuti yetu ya www.vpo.go.tz, www.daressalaam.diplo.de, www.panda.org na www.tanzania.un.org

ANGALIZO: Wafanyakazi wa taasisi zilizoandaa shindano hili pamoja na ndugu zao hawaruhusiwi kishiriki. Tangazo hili limetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF, GIZ, Ubalozi wa Ujerumani na Vodacom Foundation)        

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi