Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Masasi Yajidhatiti Kuimarisha Mawasiliano na Wananchi
Jul 26, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33890" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu akisisitiza jambo viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari-MAELEZO walipotembelea Manispaa hiyo ikiwa ni ya juhudi za kuhamasisha Maafisa Habari na Mawasiliano kutekeleza majukumu yao kwa weledi na pia kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto zinazowakabili katika Halmashauri zao na Mikoa.

[/caption] [caption id="attachment_33891" align="aligncenter" width="750"] Kiongozi Mwenza wa msafara kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari–MAELEZO, Bi. Gaudensia Simwanza akisisistiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu walipofanya ziara katika Halamashauri hiyo kuona utendaji kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali katika kuisemea Serikali.[/caption]

Na Frank Mvungi- MAELEZO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu, amesema kuwa dhamira ya Halmashauri hiyo ni kuendelea kuimarisha mawasiliano na wananchi ili waweze kufahamu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Akizungumza na ujumbe wa viongozi kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO, uliomtembelea Ofisini kwake Bi. Mkwazu amesema kuwa halmashuri hiyo inatambua umuhimu wa wananchi kupata taarifa za miradi ya maendeleo kwa wakati kupitia vyombo vya habari.

“Afisa Habari wetu anashiriki kikamilifu katika jukumu hili la kuwajulisha wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayoteklezwa na mikakati yetu ni kumuwezesha zaidi kadiri rasilimali zitakavyopatikana kwa kumpatia vitendea kazi bora ili atekeleze jukumu hili kwa ufanisi, “alisisitiza Bi. Mkwazu

[caption id="attachment_33892" align="aligncenter" width="900"] Kiongozi wa msafara kutoka Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari-MAELEZO Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wa Halmashuri ya Wilaya ya Masasi Bi mara baada ya ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo.[/caption] [caption id="attachment_33893" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari-MAELEZO walipotembelea Halmashuri hiyo kuwahamasisha Maafisa Habari na Mawasiliano kutekeleza majukumu yao kwa weledi na pia kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto zinazowakabili Maafisa habari katika Sekretarieti za Mikoa na Halmashuri.[/caption]

Mkurugenzi huyo aliielezea sekta ya mawasiliano kama nyenzo muhimu katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa wanapata elimu kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kilimo.

Aliongeza kuwa suala la mawasiliano katika Halmashauri hiyo ni limepewa kipaumbele kwa kuwa ndiyo chachu ya maendeleona wananchi wanahitaji kufahamu mipango mbalimbali ya maendeleo ya Halmashauri hiyo ili nao waweze kushiriki kikamilifu katika kutekeleza mipango hiyo.

Kwa upande wake kiongozi wa ujumbe huo Bi. Gaudensia Simwanza amesema kuwa ni wakati muafaka kwa maafisa habari na mawasiliano Serikalini kuwa na mawasiliano ya kimkakati na kuangalia namna bora ya kuwasiliana na wananchi kuhusu yale yanayoteklezwa na Serikali katika maeneo yao.

[caption id="attachment_33894" align="aligncenter" width="758"] Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Bi. Changwa Mkwazu mara baada ya ziara ya ujumbe kutoka Idara ya Habari-MAELEZO na Chama cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO).[/caption]

“Ni muhimu kwa Afisa Habari kuonesha umuhimu wa mawasiliano kwa kutekleza majukumu yake kwa weledi” alisisitiza Simwanza.

Ziara ya Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari-MAELEZO inalenga kuimarisha utendaji kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashuri hapa nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi