Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (kushoto) akisaini mkataba wa Makubaliano (Strategic Assistance Agreement ) na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas (katikati) kuhusu utoaji wa fedha dola za kimarekani milioni 224 zaidi ya Shilingi bilioni 499 tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson akishuhudia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (kushoto) akibadilishana mkataba ya makubaliano (Strategic Assistance Agreement) na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas mara baada ya tukio hilo la mkataba wa makubaliano katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.