Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Marais wa Afrika Wampongeza JPM kwa Ushindi wa Kishindo
Nov 05, 2020
Na Msemaji Mkuu

Na Anitha Jonas – Dodoma.

Marais waliyohudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli
wampongeza kwa ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliyofanyika hivi karibuni pamoja na kuwapongeza
watanzania kwa kumaliza zoezi hilo kwa amani.

Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni alisisitiza kuwa ushiriki wa nchi
mbalimbali za Afrika katika sherehe hiyo ni matunda ya msimamo thabiti wa Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage
Nyerere na baadhi ya viongozi wa Afrika ambao hawakukubali kuwa vibaraka wa mataifa ya nje.

“Napenda kutoa pongezi kwa watanzania kwa kufanya uchaguzi salama na kumaliza bila vurugu zozote pia na toa
pongezi kwa Rais Magufuli kwa ushindi wa kishindo kwani ameshinda kwa kura nyingi pamoja na wabunge mbalimbali wa
chama cha CCM nao nimewaona wameshinda kwa kura nyingi, nilikuwa nikifuatilia matangazo ya matokeo ya uchaguzi
kupitia televisheni ya TBC 1,” alisema Museveni.

Pamoja na hayo naye Rais wa Comoro, Azali Assoumani alitoa pongezi kwa Rais Magufuli huku akisisitiza kumuombea
katika majukumu yake aliyopewa ya kuwatumikia na kuwaongoza Watanzania ili aweze kukamilisha kazi hiyo kama
ilivyo desturi ya viongozi kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi kwa msaada wa Mungu.

Naye Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Emmaerson Mnangagwa alitoa pongezi kwa watanzania na kutoa salamu kutoka
wananchi wa Zimbambwe ambapo alisisitiza kuwa Zimbabwe wanaiangalia Tanzania kama baba na mama wa uhuru wa
taifa lao kama alivyowasisi Hayati Mwl. Julius Nyerere.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa sababu katika kipindi alichokuwa
Mwenyekiti wa SADC alikuwa kinara wa kusimamia kuondolewa kwa vikwazo mbalimbali ambavyo Zimbabwe tulikuwa
tumewekewa kwa kutangaza tarehe 25 Oktoba,2020 kuwa siku maalum ya kupinga vikwazo hivyo ikiwa ni maamuzi ya
Jumuiya ya SADC,” alisema Rais Mnanangwa.

Halikadhalika nae Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Botswana , Slumber Tsogwane alitoa salamu kwa niaba ya Rais wake
Mokgweetsi Masisi kwa kumpongeza Rais Magufuli kwa ushindi wa kishindo huku akieleza sababu mbalimbali

zilizomfanya rais wake ashindwe kushiriki sherehe hiyo kwa kubanwa na majukumu ya kitaifa, pamoja na hali ya
kuhitajika kukaa karantini mara baada ya kurejea nchini kwa siku kumi na nne atakapotoka nje ya nchi kutokana na hali
ya ugongwa wa Corona .

Aidha, Katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliwashukuru
watanzania kwa kujitokeza kumpigia kura kwa wingi na kumpa ushindi wa kishindo na alisisitiza kuwa uchaguzi kwa sasa
umekwisha na hivyo ni wakati wa kuchapa kazi na kulijenga taifa.

“Napenda kuwapongeza viongozi wote wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kusimamia zoezi la uchaguzi vyema
na kuhakikisha linaendeshwa kwa uwazi na haki, pia nawashukuru watanzania wote kwa kuwa wazalendo na kulinda
amani ya taifa na mara baada ya uchaguzi,” alisema Rais Magufuli.

Akiendelea kuzungumza mara baada ya uapisho huo, Rais Magufuli aliahidi kuendelea kusimamia miradi mikubwa yote
aliyoianzisha na kutekeleza mingine mipya pamoja na kuimarisha usimamizi wa rasilimali za taifa na kukuza uchumi,
ikiwemo kutatua changamoto ya ajira kwa vijana pamoja na mapambano dhidi ya rushwa.

Sherehe hizo za uapisho zilihudhuriwa na Marais watatu, Mabalozi takribani themanini, viongozi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika wakiwemo mawaziri wa nchi
mbalimbali na viongozi wa mashirika ya kimataifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi