[caption id="attachment_20756" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Miliki katika Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw.Hamed Abdallah kuhusu miradi ya ujenzi wa shirika inayoendelea katika eneo la Kijichi,Temeke,Dar es salaam. Mhe.Mabula alikuwa akikagua utendajiwa sekta ya ardhi katika ziara yake ya siku mbili Jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na.Paschal Dotto
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezitaka Manispaa na Halmashauri nchini kuongeza juhudi katika ukasanyaji kodi ya ardhi hatua inayolenga kuongeza tija ya maendeleo ya sekta hiyo.
Akizungumza katika ziara yake ya siku mbili kwa Manispaa za Kinondoni, Temeke na Ilala katika Mkoa wa Dar es Salaam Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula alisema kuwa sekta ya ardhi katika Manispaa na halmashauri mbalimbali nchini itajiendesha kwa ukusanyaji kodi kwa pango la ardhi kuwa mzuri katika Manispaa hizo.
Mabula alisema kuwa ukusanyaji kodi kwa njia ya mfumo mpya uliofungwa kwenye Manispaa ni njia bora ya kupata mapato na kuendeleza sekta ya ardhi, kwa hiyo watumishi wa idara hiyo waweke juhudi za kudai kodi hiyo hasa kwa wadaiwa sugu ambao wanadaiwa madeni makubwa ya pango la ardhi.
[caption id="attachment_20758" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Felix Lyaniva(kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula(kushoto)katika ofisi za Manispaa ya Temeke kukagua utendaji wa shughuli za sekta ya ardhi.[/caption] [caption id="attachment_20759" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula(kulia) akiangalia utendaji kazi wa mfumo mpya wa ukusanyaji kodi ya ardhi wakati wa ziara ya siku mbili Jijini Dar es Salaam.[/caption]“Katika mfumo huu wa kodi na nimeona baadhi ya takwimu kwa wateja wanaodaiwa, kati ya wateja 35,000 nimechukua wateja 100 wanaodaiwa kuanzia 5,000,000 na jumla yao ni bilioni 13 kwa hiyo tukiweza kuwadai tutapata pesa nyingi tu”, alisema Mabula.
Aidha Mabula alisema kuwa juhudi za ukusanyaji kodi zimerahisishwa kwani mfumo huo mpya utawawezesha watumishi katika idara ya ardhi kupata takwimu kwa urahisi na kuweza kupata majina ya wadaiwa sugu.
Aliongeza kuwa Maafisa ardhi hawana budi kutumia mfumo huo mpya kwa kuwa hauhitaji muda mwingi kutafuta taarifa katika mafaili yaliyopo masijala kwa ajili ya kukagua takwimu na kwa kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha makusanyo ya kodi ya ardhi.
Akiwa katika Manispaa ya Ilala, Mabula aliwataka watumishi wa manispaa hiyo kuwa na umoja baina yao na baraza la madiwani wa baraza la manispaa hiyo ili kuweza kushirikiana na kuongeza juhudi za ukusanyaji mapato..
Aidha katika ziara hiyo Mabula aliwataka Wakuu wa Wilaya kutoa taarifa kwa Serikali iwapo kutakuwa na uhaba wa watumishi hususani katika maeneo yenye uhitaji mkubwa na Wizara iangalie namna ya kuwapa watumishi na kurahisiha utendaji kazi.