Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mamia Washiriki Mazishi ya Dada wa Rais Magufuli Bi. Monica Joseph Magufuli Chato, Geita
Aug 21, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_34420" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.[/caption] [caption id="attachment_34421" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.[/caption]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aongoza Mamia ya Wakazi wa Chato katika Mazishi ya Dada yake Marehemu Monica Magufuli yaliyofanyika Chato Mkoani Geita.Agosti 21,2018

Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aitwaye Monica Joseph Magufuli aliyefariki dunia Jumapili tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza amezikwa leo katika makaburi ya familia yaliyopo katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

[caption id="attachment_34422" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.[/caption] [caption id="attachment_34423" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.[/caption]

Misa Takatifu ya Mazishi ya Monica Joseph Magufuli imeongozwa na Askofu Jimbo Katoliki la Rulenge Mhashamu Severine Niwemugizi aliyeambatana na Maaskofu wengine saba, pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mhe. Raila Amolo Odinga, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mawaziri, Wabunge, Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wengine mbalimbali wa Mikoa, Wilaya, Taasisi, Idara na Kampuni.

[caption id="attachment_34424" align="aligncenter" width="750"] Jeneza lenye mwili wa marehemu Monica Joseph Magufuli likipelekwa Kanisani kwa ajili ya Misa takatifu Chato Mkoani Geita.[/caption] [caption id="attachment_34425" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.[/caption] [caption id="attachment_34426" align="aligncenter" width="750"] Baba Askofu mkuu Mwandamizi Yuda Thaddeus Ruwaichi akiongoza Misa ya kumuombea Marehemu Monica Magufuli Chato mkoani Geita[/caption]

Katika salamu zake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi na wananchi wote walijitokeza kuungana na familia katika kumsindikiza Dada yake katika safari yake ya mwisho na amesema familia inatambua upendo, heshima na mshikamano mkubwa ambao wameuonesha kwao. “Mmetuonesha upendo mkubwa sana na kweli ujio wenu na kuungana nasi katika tukio hili mmetufariji sana, asante sana kwa upendo huu na Mungu awabariki sana” amesema Mhe. Rais Magufuli.

[caption id="attachment_34427" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkewe Mama Marry Majaliwa wakitoa heshma zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.[/caption] [caption id="attachment_34428" align="aligncenter" width="750"] Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.[/caption] [caption id="attachment_34429" align="aligncenter" width="750"] Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi