Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mameneja, Watunga Sera Uhifadhi Wanyamapori Wapewa Kibarua Kizito.
Dec 09, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24487" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akimkabidhi kitabu Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori cha Serengeti, Dkt.Robert Fyumagwa mara baada ya hafla iliyofanyika jana jijini Arusha ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea hali ya bioanuwai kabla ya ujenzi wa barabara itakayoanzia Mto wa Mbu kwenda Natron hadi Loliondo itakayoruka kipande katika hifadhi ya Serengeti hadi Mugumu. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Prof. Apolinaria Pereka (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa Wizara Dkt. Iddi Mfunda.[/caption]

Katibu Mkuu  wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi  amewataka Mameneja pamoja na Watunga sera za uhifadhi wa Wanyamapori waanze kuyafanyia kazi matokeo ya tafiti 186  zilizowasilishwa na wanasayansi watafiti wa uhifadhi  ili zilete tija kwa taifa

Amewataka Mameneja na Watunga sera hao kuacha tabia ya kuzifungia tafiti hizo kwenye makabati badala yake wazisome ili waweze kuzitumia katika kujibu changamoto zilizojitokeza kwenye uhifadhi.

Milanzi amesema kuwa masuala   yaliyoibuliwa  kwenye  tafiti  hizo yaanze  kutafutiwa ufumbuzi yasisubili hadi matatizo yatokee.

[caption id="attachment_24484" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Prof. Apolinaria Pereka pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TAWIRI, Simon Mduma (wa pili kulia) mara baada ya kufunga mkutano wa kumi na moja wa wanasayansi watafiti wa wanyamapori wa kutoka ndani na nje ya nchi uliofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arusha.[/caption]

Alibainisha hayo jana mjini Arusha  wakati alipokuwa akifunga  Mkutano wa kimataifa wa kumi na moja wa  wanasayansi watafiti wa uhifadhi wa wanyamapori, mazingira pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) umefanyika kwa muda wa siku tatu ambapo wanasayansi watafiti wa kutoka ndani na nje ya nchi waliwasilisha na kujadili tafiti 186 katika maeneo hayo.

Aidha, Milanzi amezitaka Taasisi na Mashirika binafsi kuiga mfano wa TAWIRI ya kuandaa mikutano inayowakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali Duniani hali inayopelekea kuvitangaza vivutio vya utalii pamoja na kukua kwa utalii wa mikutano.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha Utalii wa mikutano inaanza kuchukua nafasi kwa kulingiizia Taifa mapato yatokanayo na wageni wanaokuja kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya kimataifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TAWIRI, Prof. Aporinalia Peleka amesema mkutano huo umetoa fursa kwa wahifadhi pamoja na watunga sera kuziona changamoto zinazoikabili nchi katika masuala ya uhifadhi.

Aliongeza kuwa, tafiti hizo zilizowasilishwa zitaisaidia Serikali kupanga mipango yake ya muda mrefu na muda mfupi kulingana na matokeo ya tafiti zilivyojitokeza.

Aidha, amezitaka taasisi na mashirika binafsi kuzitumia tafiti hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Mkutano huo ulifunguliwa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambapo alizitaka taasisi za Serikali pamoja na mashirika binafsi ziisaidie TAWIRI ili iweze kufanya tafiti tofauti na inavyofanya sasa.

     

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi