Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mama Samia Legal Aid Yawafikia Watu 383, 293 Nchini
Feb 01, 2024
Mama Samia Legal Aid Yawafikia Watu 383, 293 Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Chinangali kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.
Na Jonas Kamaleki – Dodoma

Kampeni ya Mama Samia Legal Aid imewafikia watu 383, 293 katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu, ambapo migogoro takribani 511 imetatuliwa na imesaidia kubaini ni maeneo ya nchi yenye migogoro zaidi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yalifonyika katika viwanja vya Chinangali jijini humo.

“Naiagiza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na wadau, kutekeleza kikamilifu mfumo wa utoaji wa msaada wa kisheria kwa mujibu wa sheria zilivyo kwenye maeneo yenye malalamiko mengi ambayo ni ardhi, matunzo ya watoto, ndoa, mirathi, ukatili wa kijinsia na madai”, alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kuwa, jitihada kubwa zimefanyika na zinaendelea katika kuimarisha mfumo wa haki jinai nchini, serikali inaweka mkazo kwenye mfumo wa haki madai, ambapo tumebaini malalamiko kwani kesi zinacheleweshwa, mzunguko ni mkubwa wenye hatua kadha wa kadha, hii inapoteza muda kwani unahusisha ufuatiliaji mrefu. Hivyo, naagiza kufanyika maboresho ili haki madai ipatikane kwa uharaka ikiwemo kesi za kibiashara na uwekezaji.

Rais Samia amezitaka Mahakama kutoa haki kwa watu wote bila kujali hali za watu kijamii, kiimani na kiuchumi, kutocholewesha haki bila sababu ya msingi.

“Nashauri mahakama ziwe msitari wa mbele katika kukuza na kuendeleza usuluhishi wa migogoro na mashauri yaishe mapema bila kuathiri ubora wa hukumu zinazotolewa.  Kazi ya kutoa haki ni ya Mungu, hivyo waheshimiwa majaji na mahakimu mnawajibika kuifanya kwa uadilifu mkubwa, msitoe hukumu kwa dhuluma”, alishauri Rais Samia.

Aidha, Rais Samia alisema kuwa ongezeko la imani ya wadau wa haki kwenu kutoka 65% mwaka 2015 hadi 88 % mwaka 2023, ni ushahidi tosha kwamba mnafanya kazi kubwa na kwamba mahakama inakwenda na mabadiliko, na ndiyo maana idadi ya watumiaji wa mahakama inaongezeka.

“Nawapongeza Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa maoni, mapendekezo na maombi yaliyopevuka kupitia rais wenu wa chama, Wakili Harold Sungusia, hii inaonesha kuwa mmekua na kukomaa katika utendaji kazi wenu”, alipongeza Rais Samia.

 Pamoja na uwekezaji mkubwa wa TEHAMA kwenye mahakama serikali imeendelea kuimarisha utendaji wa mahakama kwa ujenzi wa majengo ya kisasa kama vile vituo jumuishi vya kutolea haki, kuongeza idadi ya watenda kazi.

 Kwa sasa nchini imefanikiwa kuongeza idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani kutoka 16 mw

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi