Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Malawi Yavutiwa na Matibabu ya Kibingwa MOI
Mar 22, 2018
Na Msemaji Mkuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi Dkt.  Charles Mwansambo (kulia) akikaribishwa na Meneja wa huduma za uuguzi  wa MOI Elizabeth mbaga katika vyumba vya kisasa vya kulipia vya MOI  wakati wa ziara yake iliyolenga kujifunza namna Taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.

Katibu Mkuu  Wizara ya Afya nchini Malawi Dkt.  Charles Mwansambo akiwa katika kikao na viongozi waandamizi wa  Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) katika ukumbi wa mikutano (Board room) mara baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo kwa ziara iliyolenga kujifunza namna Taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake  mapema jana.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi Dkt.  Charles Mwansambo (wapili kutoka kulia)   akitoa neno la Shukrani kwa viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya ziara yake katika Taasisi hiyo mapema jana.

Kaimu Mkuu wa  Idara ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)  Bw. Juma Rehani akimpa maelezo Dkt. Charles Mwansambo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi, kuhusu namna  vyumba vya upasuaji vinavyofanya kazi katika Taasisi hiyo wakati wa ziara iliyolenga kujifunza namna Taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.

Na Mwandishi  Wetu

Katibu Mkuu  Wizara ya Afya ya Malawi Dkt. Charles Mwansambo  ametembelea Taasisi ya  Tiba ya Mifupa Muhimbili  (MOI) ili kupata uzoefu wa namna Taasisi hiyo inavyotoa huduma za kibobezi (super specialist).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo Jijini Dar es Salaam Dkt. Mwansambo amesema ametembelea MOI ili kuona uwezekano wa kuwaleta wagonjwa wa Malawi kupata huduma za Kibingwa za Mifupa, Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu badala yakuwapeleka India.

" Nimefurahi kuona kuwa tuna huduma nzuri za kibingwa kwa jirani zetu wa Tanzania, hili ni jambo jema na litatupunguzia gharama za kuwapeleka wagonjwa India badala yake tunawaleta hapa MOI" amesema Dkt.Mwansambo.

 Aidha, Dkt. Mwansambo alipata fursa ya kutembelea vyumba vya upasuaji vya MOI, vyumba vya wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU), wodi za watoto na wodi maalum za kisasa za kulipia.

 Kutokana na mafanikio ya miundo mbinu ya kisasa yaliyopo MOI Dkt. Mwansambo ameonyesha dhamira ya dhati ya kuleta madaktari wanafunzi hapa  ili wapate ujuzi wa zaidi.

 Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI  Mhandisi .Reginald Kimambo alimueleza Dkt. Mwansambo kwamba huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo zimebobea katika  Mifupa, Ajali, Upasuaji wa ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu pamoja na kutua  mafunzo kwa madaktari bingwa wa COSESCA.

Ziara hii imekuja baada ya mkutano wa 65 wa Mawaziri wa  Afya wa Ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi