Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais wa Cuba Awasili Nchini kwa Ziara ya Kikazi
Jan 23, 2024
Makamu wa Rais wa Cuba Awasili Nchini kwa Ziara ya Kikazi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valdés Mesa mara baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki. Mhe. Salvador Valdés Mesa amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 Januari, 2024.
Na Mwandishi Wetu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valdés Mesa amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 Januari, 2024.

Mara baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Mesa alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki.

Akiwa nchini, Mhe. Mesa atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, pia atatembelea taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Mhe. Mesa pia atatembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere pamoja na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa za viuadudu ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi