Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais: Serikali Haitolala Mapambano dhidi ya Rushwa, Ufisadi
Jun 22, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4142" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa zamani wa Georgia, Mhe. Mikheil Saakshvili (kushoto) kabla ya Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).[/caption]

Na Mwandishi Wetu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa  Serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapo koma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika katika Kituo cha Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni kipaumbele cha kwanza katika Serikali ya awamu ya Tano na wale wote wanaowezesha, kunufaika na kuhusika na vitendo hivyo wataendelea kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo nchini.

[caption id="attachment_4144" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).[/caption]

“Kupambana na rushwa ni jambo la msingi na muhimu kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu katika nchi yeyote Duniani,” amesisitiza Makamu wa Rais.

Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu Tano chini ya Uongozi Shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, inaendelea kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa muda mrefu sasa imechangia kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Amesema Serikali ya Tanzania inalenga kufikia kipato cha kati na kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2025 hivyo malengo hayo yatafanikiwa  haraka iwapo tu vitendo vya rushwa vitakomeshwa katika ngazi zote nchini.

“Rushwa ni mbaya na imeharibu sana maisha ya watu na maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, hivyo ni lazima ikomeshwe  ili jamii iishi maisha mazuri”, ameeleza Makamu wa Rais.

[caption id="attachment_4143" align="aligncenter" width="750"] Rais wa zamani wa Georgia, Mhe. Mikheil Saakshvili akihutubia na kutoa uzoefu wa nchi yake dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).[/caption]

Amesema kuwa hakuna nchi yeyote duniani ambayo haijagushwa na misukosuko ya vitendo vya rushwa lakini Bara la Afrika limeendelea kuteseka na vitendo hivyo kwa miongo kadhaa sasa, hivyo jitihada za pamoja zinatakiwa katika kutokomeza vitendo hivyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.  Angellah Kairuki amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa wizara yake itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao ya kazi.

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano za kupambana na vitendo vya rushwa na kusisitiza kuwa benki hiyo ataendelea kutoa mchango wake wa hali na mali katika kuisaidia Tanzania katika uimarishaji wa mapambano hayo.

Mkutano huo wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa unahudhuriwa na viongozi mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wenye uelewa na uzoefu katika mapambano dhidi ya rushwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi