Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Azindua Mashine za Mionzi Ocean Road
Mar 29, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41529" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo na mashine za tiba ya saratani.[/caption]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la saratani kwa Watanzania linaweza kupungua ama kuondokana nalo endapo kutakuwa na tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa jengo na mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC ambazo ni za kisasa kabisa na kwa Afrika, Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuwa nazo.

tunaweza kujikinga kwa kufuata kanuni za afya zinavyotuelekeza kula chakula bora, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kuepuka kunywa pombe kupita kiasi na kuepuka matumizi ya tumbaku”alisema Makamu wa Rais.

Mradi wa ununuzi na ufungaji wa mashine mpya za kisasa za tiba ya mionzi umegharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo shilingi bilioni 9.5 zimetumika.

[caption id="attachment_41530" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (hawapo Pichani), kabla ya uzinduzi wa mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC, uliofanyika leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kathe Kamba, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage.[/caption] [caption id="attachment_41531" align="aligncenter" width="889"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kufungua mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC, leo katika Taasisi ya Saratani Ocaen Road, Dar es Salaam[/caption]

Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha huduma za saratani hasa huduma za Kinga, Uchunguzi na Matibabu ya awali ikiwemo kuongeza vituo vya upimaji wa dalili za awali za Saratani ya mlango wa kizazi na matiti ambapo jumla ya vituo 650 vinatoa huduma hii kwa wakati.

Makamu wa Rais amewataka  wananchi wote hasa wanawake kufika katika vituo ili kufanyiwa uchunguzi  kwani zikigundulika dalili za awali mgonjwa atatibiwa na kupona.

Pia Makamu wa Rais amesisitiza wanaume waanze kuchukua mwamko wa kupima afya  zao hasa kupima saratani ya tezi dume.

Nashukuru Wizara kwa kuanzisha kampeni ya upimaji wa virusi vya ukimwi kwa wanaume, kwa kauli mbiu ya Furaha Yangu na ingefaa suala hili liende pia kwa upimaji wa Saratani ya Tezi Dume” alisisitiza Makamu wa Rais.

[caption id="attachment_41532" align="aligncenter" width="1000"] Moja ya Mashine za tiba ya mionzi LINAC (CT-STIMULATOR) iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Raod, Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Mwisho, Makamu wa Rais ameupongeza mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuingiza matibabu ya Saratani katika huduma ambazo wanagharimia“Ningependa kuwaagiza mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhakikisha wanagharimia huduma hii ya tiba ya mionzi kwa LINAC.”

Wakati huohuo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema katika kipindi kifupi cha miaka mitatu sekta ya Afya imepata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo  chanjo kwa watoto zimefikia asilimia 98%, upatikanaji wa dawa muhimu ni asilimia 95%, vifaa na vifaa tiba, huduma za mama na mtoto ikiwemo ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya.

“Tumekusudia  kuleta watalii wa matibabu”alisema Waziri Ummy.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi