Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tumieni Malighafi za Nchini Katika Viwanda Vyenu- Makamu wa Rais
Nov 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_22504" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakati wa hafla ya kuzindua rasmi Kongamano na Maonesho ya Wafanya Biashara na Wajasiriamali wa Afrika Mashariki leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa EAC Balozi Liberat Mfumukeko, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara na wajasiriamali wa Afrika Mashariki(EABC) na Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo Felix Mosha. Maonyesho hayo ya siku tatu yameanza leo tarehe 14 -16 Novemba yameandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC). (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Na: Jonas Kamaleki

Serikali imezitaka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki kutumia malighafi zinazopatikana katika nchi hizo kwa ajili ya viwanda badala ya kuagiza nje.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Biashara na Ujasiriamali ya Afrika Mashariki.

[caption id="attachment_22505" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuzindua rasmi Kongamano na Maonesho ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Afrika Mashariki leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Liberat Mfumukeko, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara na wajasiriamali wa Afrika Mashariki(EABC) na Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo Felix Mosha. Maonyesho hayo ya siku tatu yameanza leo tarehe 14 -16 Novemba yameandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC).[/caption] [caption id="attachment_22506" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)Balozi Liberat Mfumukeko akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kongamano na Maonesho ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Afrika Mashariki leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara na wajasiriamali wa Afrika Mashariki(EABC) na Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo Felix Mosha. Maonyesho hayo ya siku tatu yameanza leo tarehe 14 -16 Novemba yameandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC).[/caption]

“Ndoto yetu ya uchumi wa viwanda sio kuhamishia viwanda vya nje hapa nchini bali ni kuwa wabunifu na kujenga viwanda vyetu wenyewe,”amesema Samia.

Amesema ujenzi wa uchumi wa viwanda uendane na kufanya kilimo chenye tija ambacho kinalenga kuwaondolea umaskini wananchi.

“Wakulima wetu hawana uhakika na soko la mazao yao kwani wanapopata mazao kwa wingi, bei inashuka, wakati wa ukame mazao yanaharibika, hivyo kwao nyakati zote ni taabu,” amesema Mhe. Samia.

[caption id="attachment_22510" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akitembelea baadhi ya mabanda ya wajasiriamali mara baada ya kuzindua rasmi Kongamano na Maonesho ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Afrika Mashariki leo Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku tatu yameanza leo tarehe 14 -16 Novemba yameandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC).[/caption]

Makamu wa Rais amewataka wakulima waongeze thamani ya mazao yao badala ya kuuza mazao ghafi. Kwa kufanya hivyo watajiongezea kipato na kuondokana na umaskini, aliongeza Samia.

Uanzishwaji wa viwanda katika Jumuiya ya Afrika mashariki utasaidia katika kuinua kilimo kwani mazao hayo yatapata uhakika wa soka kwenye viwanda hivyo.

Amezitaka nchi hizo kutengeneza ajira hasa kwa vijana ambao takwimu zinaonyesha kuwa ndio wengi, hivyo ni muhimu kuwapa kipaumbele.

Serikali na sekta binafsi zimetakiwa kufanya juhudi za makusudi kuanzisha viwanda ambavyo vitaongeza ajira na kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda.

[caption id="attachment_22511" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali wanawake kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuzindua rasmi Kongamano na Maonyesho ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Afrika Mashariki leo Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku tatu yameanza leo tarehe 14 -16 Novemba yameandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC). (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Aidha, Mhe. Samia amezitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kudumisha amani kwani bila amani uwekezaji katika viwanda na maeneo mengine hauwezekeni.

Amani ni bidhaa adimu ambayo inapatikana kwa gharama, hivyo siyo ya kuchezea bali ni ya kulindwa, aliongeza Mhe. Samia.

Huu ni Mkutano wa Pili ambao unajumuisha washiriki kutoka, Kenya, Burundi, Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania. Katika Mkutano huo yanafanyika maonyesho ya wajasiriamali kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashiriki.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi