Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Amuwakilisha Rais Magufuli kwenye Kuapishwa Rais Mpya wa Burundi
Jun 19, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53389" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya kumuwaklilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye leo Juni 18, 2020. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwa.[/caption]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alikuwa miongoni mwa Viongozi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Burundi, Evariste Ndayishimiye zilizofanyika jana katika Mji wa Gitega, Uwanja wa  Igoma Stadium Nchini Burundi.

Katika sherehe hizo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akitoa salam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. samia Suluhu Hassan , amempongeza Rais Ndayishimiye kwa ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa hivi karibuni na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Burundi katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

[caption id="attachment_53391" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye leo Juni 18, 2020. kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete.[/caption] [caption id="attachment_53393" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye leo Juni 18, 2020.[/caption]

Makamu wa Rais Mhe. Samia pia aliwapa pole Wananchi wa Burundi kwa kwa msiba mkubwa wa aliyekuwa Rais wa Nchi yao marehemu Pierre Nkurunziza na kuwataka wawe na subira katika kipindi hiki cha maombolezo.

Aidha, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Damas Ndumbaro walipata nafasi ya kufika nyumbani kwa marehemu Nkurunziza Jijini Bujumbura kwa ajili ya kuitembelea na kuifariji familia akiwemo mjane na watoto wa marehemu, ambapo amemuomba kwa Mwenyezi Mungu kuwapa uvumilivu na kuwa na subira katika kipindi hiki cha maombolezo.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amerejea Nchini akitokea Nchini Burundi jana Usiku.

[caption id="attachment_53394" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakati Rais Ndayishimiye alipokuwa akipokea Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Burundi baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18, 2020 katika Uwanja wa Igoma Stadium Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shughuli hiyo.[/caption] [caption id="attachment_53395" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jarmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye mara baada ya Rais Ndayishimiye kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Stadium Nchini Burundi ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete.[/caption] [caption id="attachment_53392" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega nchini Burundi leo Juni 18, 2020.[/caption] [caption id="attachment_53390" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye,kushoto ni Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwa na kutoka kulia ni Rais  Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete  Ikulu ndogo Gitega nchini Burundi leo Juni 18, 2020.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi