Makamu wa Rais Kuelekea Nairobi Mazishi ya Rais Mstaafu Mwai Kibaki
Apr 29, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Aprili 2022 akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akiondoka kuelekea Nairobi nchini Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Mwai Kibaki.