Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Azungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden
Jun 03, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 3 Juni 2022 amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Mhe. Ann Linde, mazungumzo yaliyofanyika mjini Stockholm nchini Sweden.

Makamu wa Rais amesema Tanzania na Sweden zimekua na ushirikiano mzuri wa muda mrefu na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuimarisha uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili. 

Aidha, ameishukuru Serikali ya Sweden kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo za Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu, Biashara pamoja na  Haki za Binadamu.

Makamu wa Rais amesema nchi ya  Sweden imepiga hatua katika sekta ya Afya hasa kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo na kusema ipo hajaya mataifa hayo kushirikiana katika kutoa mafunzokwa madaktari wa Tanzania.

 Ameongeza kwamba mataifa hayo mawili yanaweza kurejesha ushirikiano uliokuwepo hapo awali katika sekta ya Elimu ya juu uliochochea upatikanaji wa wataalamu mbalimbali nchini Tanzania.

Pia, Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu yasita inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katikakuboresha mazingira ya uwekezaji, kuimarisha sekta ya viwanda, uhifadhi wa mazingira, kuimarisha sekta ya kilimo pamoja na kuwekeza katika huduma za kijamii kama vile Elimu na Afya.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Ann Linde ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua mbalimbali inazoendelea kuchukua ikiwemo kuimarika kwa haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari  pamoja na demokrasia. 


Aidha, amesema Serikali ya Tanzania imefanya jambo la muhimu kutoa haki kwa wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo kwa kutambua elimu ndio nguzo muhimu kwa maisha yao. 

Waziri Linde amesema upo uwezekano wa Tanzania na Sweden kuongeza zaidi ushirikiano hasa wakibiashara kwa manufaa ya mataifa yote mawilikutokana na uwepo wa miundombinu kama reli namabasi yaendayo haraka nchini Tanzania.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango yupo nchini Sweden kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 wenye lengo la kuchochea utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Umoja waMataifa (Ajenda 2030) hususani katika upande wa mazingira na kujadili namna ya kurejesha uchumi endelevu katika kukabiliana na  janga la Uviko 19.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi