Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA MAJI WA BILIONI 29 MKOANI TABORA.
Apr 29, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Serikali imezindua mradi wa ujenzi na usambazaji maji vijijini wenye thamani ya shilingi bilioni 29 katika Halmashauri saba za mkoani Tabora.

Mradi huo umezinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Kijiji cha Mabama Wilayani Uyui mkoani Tabora.

Ujenzi wa Mradi huo umefadhiliwa na Japan kupitia  Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) ambao umewezesha uchimbaji wa visima 111 na ujenzi wa mitandao minne ya bomba.

Akizungumza na wananchi wa Mabama mkoani Tabora wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo Makamu wa Rais huyo alisema kuwa ujenzi wa mradi huo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wengi hapa nchini na wale wa mkoa huo wanakuwa na uhakika wa huduma ya maji safi na salama.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuendelea na jitihada kuwajenga miradi mbalimbali wananchi kwa nguvu zake na wakati mwingine kwa kushirikiana na wahisani.

Mhe. Samia alisema kwa kuwa mradi huo utawanufaisha wanachi wapatao 40,352 katika vijijini 31 vya Mkoa wa Tabora ni vema wananchi wakautunza ili uweze kutumika kwa muda mrefu.

Aliwaasa wanufaika wa mradi huo maji vijijini kutoharibu miundo mbinu za visima na bomba ili uweze kusaidia kuwaondolea adha wananchi na hasa wakinamama na watoto wa kike ambao walikuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kushiriki katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.

Aidha , Makamu huyo wa Rais ametoa kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili jamii iendele kunufaika na rasimali hiyo muhimu kwa uhai wa wanandamu na maendeleo mengine.

Aidha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano huyo ameishukuru serikali ya Japani kwa msaada huo ambao ni ukumbozi kwa wakazi wa Tabora.

Hivyo kufuatia hali hiyo aliwaagiza viongozi kuanzia ngazi ya chini hadi Mkoa kutomfumbia macho mtu anayeharibu mazingira kwa makusudi na ikiwezekana hatua kali zoichukuliwe dhidi yake.

Naye Balozi wa Japani hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida alisema kuwa Japan itandelea kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa miradi mbambali hapa nchini kwa lengo la kuwaletea huduma wananchi kwa karibuni.

Alisema kuwa ujenzi wa mradi huo ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo mbaina ya Tanzania na Japan na kuahidi kuendelea na ushirikiano huo.

Awamu Mkuu Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alitoa salamu za Mkoa alisema kuwa uharibifu wa mazingira mkoani huo kwa sababu za kilimo cha tumbaku kisichozingatia matumizi madogo ya kuni na ufugaji wa usiozingatia utunzaji wa mazingira umesababisha upungufu wa mvua mkoani huo.

Alisema kuwa wakati mazingira mkoani bado hayajaharibiwa mkoa huo ulikuwa na uwezo wa kupata mvua kufikia milimita 1800 lakini hivi sasa Tabora inapata mvua ambazo ni milimita 650.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa Mazingira, viongozi mbalimbali wa mkoani huo wameendesha kampeni ya kupata miti katika maeneo yote kwa kutumia teknolojia ya matone.

Naye Waziri wa  Maji na Uwagiliaji Greyson Lwenge alitoa wito kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote hapa nchini kuanzisha miradi ya uchumbiaji wa mabawa madogo madogo kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la maji katika maeneo yao.

Alisema kuwa Wizara hiyo itaendelea na jitihada zake za utatizi wa kero ya maji , lakini vema na Halmashauri zitafuta njia za kuwaondolea wananchim kero hiyo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban alisema kuwa mradi huo umekuwa mkombozi kwa baadhi ya wakazi wa mkoa wa Tabora na hasa Halmashauri yake kwa kuwa walitumia muda mwingi na fedha nyingi kununulia maji.

Alisema kuwa baada kujengwa mradi huo hivi sasa wananchi wananunua dumu moja la lita ishirini kwa shilingi 50 wakati hapo awali walikuwa wakinunua kwa kiwango cha kuanzia shilingi 500 hadi 1,000 wakati wa kiangazi.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa mradi huo pia umesaidia kupunguza muda mwingi ambao wakinamama waliupoteza kutafuta maisha badala ya kwenda kuzalisha mali.

Aliongeza kuwa faida nyingine ni kuwa mradi huo umesaidia kurudisha mahusiano katika familia.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi