Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo tarehe 26 Mei 2022 akitokea Davos nchini Uswisi alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani.