Makamu wa Rais Ashiriki Mkutano wa UNEP Nairobi Kenya, Azungumza na Rais wa Kenya
Mar 03, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango leo tarehe 3 Machi, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo (tete a tete) na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta, mazungumzo yaliofanyika kando ya Ukumbi wa Mikutano wa Shiirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) Jijini Nairobi, Kenya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango leo tarehe 3 Machi, 2022 akishiriki Mkutano maalum wa kuadhimisha miaka 50 ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) unaofanyika katika Makao Makuu yake Jijini Nairobi, Kenya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango leo tarehe 3 Machi, 2022 akitoa salamu za Tanzania kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano maalum wa miaka 50 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika hilo Jijini Nairobi, Kenya.