Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Ashiriki Misa Takatifu ya Mwaka Mpya
Jan 01, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip
Mpango akizungumza na waumini mara baada ya kumalizika kwa Misa
Takatifu ya sherehe za Bikira Maria mama wa Mungu pamoja na
kumshukuru Mungu kwa mwaka mpya 2022 katika kanisa katoliki
parokia ya mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu la Dodoma leo
tarehe 1 Januari 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip
Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 1
Januari 2022 wameungana na waumini wa kanisa katoliki parokia ya
mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu la Dodoma kushiriki Misa
Takatifu ya sherehe za Bikira Maria mama wa Mungu pamoja na
kumshukuru Mungu kwa mwaka mpya 2022. Misa hiyo imeongozwa na
Paroko wa parokia hiyo Vicar General, Onesmo Wisi.

Akizungumza na waumini hao mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo
Makamu wa Rais Dkt. Mpango amewasihi waumini na watanzania wote
kuendelea kumshukuru Mungu kwa kuvuka salama mwaka 2021 kwa
kuwa mwaka huo ulikuwa na changamoto nyingi zikiwemo za maradhi
ya Uviko19. Amewaomba waumini hao kuendelea kuliombea taifa
pamoja na viongozi wake ili waweze kuongozwa na hekima ya Mungu
katika kuwatumikia watanzania.

Makamu wa Rais amewataka watanzania kwa mwaka 2022 kufanya kazi
kwa bidii kwa kuwa hata vitabu vya dini vinasisitiza juu ya kazi na
Mungu huweka baraka kwa wale wafanyao kazi. Amesema hakuna
maendeleo yanayoweza kutokea pasipo kufanya kazi.

Aidha Makamu wa Rais amesema ni muhimu kutumia mvua
zinazoendelea kunyeesha kupanda mazao ya muda mfupi na mudamrefu kulingana na maeneo husika. Amewasihi wananchi wa Dodoma
pia kutumia mvua hizo kupanda miti katika maeneo yao ili kulinda
mazingira pamoja nakuupendezesha mkoa wa Dodoma uliokabiliwa na
upungufu wa mvua kwa muda mrefu.

Amesema wazazi wanapaswa kuwaongoza watoto wao na kuwalea
katika maadili mema ikiwemo kukabiliana na matumizi mabaya ya
mitandao ya kijamii. Amewatakia watanzania wote kuwa na mwaka
2022 wenye Amani na kusisitiza kila mmoja akatimize wajibu wake kwa
Mungu na kwa Tanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi