Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Makamu wa Rais Akutana na Prince William Jijini London
Apr 17, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30473" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Prince Williams leo katika Jumba la Kifalme la Buckingham Palace ikiwa sehemu ya ratiba zake jijini London ambapo anamuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya za Madola.[/caption]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Prince William katika jumba la Kifalme la Buckingham Palace.

Makamu wa Rais alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbali mbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado hatujawa na tekinolojia yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini tumeendelea kuimarisha ulinzi wa wanyama pori.

[caption id="attachment_30474" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimbidhi picha ya kuchorwa Prince Williams leo katika Jumba la Kifalme la Buckingham Palace kama zawadi na ishara ya kutambua mchango wa Prince William katika kupambana na ujangili, Makamu wa Rais yupo jijini London kumuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya za Madola. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)[/caption]

Kwa upande wake Prince Williams alimuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na pia Prince William amemualika Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano unaohusu masuala ya Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu jijini London.

Makamu wa Rais Mhe. Samia yupo nchini Uingereza kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.​

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi