[caption id="attachment_45936" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa, akipata maelezo kuhusu ya Reli ya Kisasa kutoka kwa Afisa Habari wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk alipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania(TRC) katika maonesho ya Wiki ya Viwanda SADC, yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa.[/caption] [caption id="attachment_45935" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa, akiangalia ramani ya Reli ya Kisasa alipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania(TRC) katika maonesho ya Wiki ya Viwanda SADC, yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa.[/caption]
Na Paschal Dotto-MAELEZO
06-08-2019
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuchangamkia fursa zitokanazo na maonesho ya Viwanda ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ili kuwezesha ukuaji wa uchumi wa viwanda ambao Serikali inaujenga.
Akizungumza wakati wa kutembelea maonesho hayo yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja vya Karimjee na Gymkana, Waziri Mkuu amesema kuwa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC yamekamilika yakihusisha kuwepo kwa maonesho ambayo nchi wanachama wataonesha teknoloji, Ubunifu na bidhaa zao kutoka katika Viwanda vya nchi za SADC.
Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imetoa fursa kwa wafanyabiashara Wakubwa, wa kati, wadogowadogo na wenye bidhaa zinazozalishwa kwa mikono kuja kuonesha na kuchukua teknolojia kutoka nchi wageni ambao wapo nchini kwa maonesho hayo ya wiki moja.
[caption id="attachment_45934" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akionyeshwa kitu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Palamagamba Kabudi (aliyenyoosha mkono) alipotembelea maonesho ya Wiki ya Viwanda SADC, yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, kushoto kwao ni Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa.[/caption]“Sisi kama Serikali tumetoa Fursa kwa wale ambao wanafanya kazi na kuzalisha bidhaa zao kwa kutumia mikono kuja kuonesha bidhaa zao ili ziweze kupata masoko kwa nchi wanachama wa SADC kwani nchi zote zinakuja hapa kuleta bidhaa mbalimbali kwa hiyo watanzania wanatakiwa kutumia fursa hii kuwauzia wageni bidhaa zetu”, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Alisema kuwa Fursa ambayo watanzania wameipata kutokana na mkutano huo wa SADC itawawezesha kukuza mitaji kwa kuungana na wageni ili kujenga viwanda vikubwa na kuimarisha uzalishaji wa bidhaa zitakazokidhi soko la nchii wanachama wa SADC.
Majaliwa alisema kuwa Maonesho hayo ni muhimu kwani yamezikutanisha nchi za SADC kuja Tanzania kuonesha bidhaa, teknolojia ya uzalishaji viwandani, pamoja na ubunifu katika kuzalisha bidhaa hizo, kwa watanzania ambao hawajawahi kufika Namibia, Msumbiji, Malawi pamoja na Nchi zingine za kusini mwa afrika ni fursa kubwa kwao kuleta bidhaa zao ili ziweze kupata soko kutoka SADC.
“Maonesho haya ya wiki ya Viwanda kutoka Nchi wanachama wa SADC yanafursa nyingi kwa watanzania kwani yatafungua milango mingi ya masoko kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, pia yatakuwa ya wazi kwa hiyo watanzania wanatakiwa kutumia fursa hii kubwa kuona bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini na nchi wanachama kutoka Jumuiya hii”, Kassimu Majaliwa, Waziri Mkuu Tanzania.
Waziri Mkuu, alisema kuwa yako mataifa ambayo yameleta bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo na madawa mbalimbali, kwa hiyo fursa ni pana kwa watanzania na ambayo ikitumiwa ipasavyo kuelekea uchumi wa kati wenye viwanda itawezesha kuinua uchumi kwa wananchi, na sasa inawakakaribisha wageni kuja kuwekeza katika sekta za madini na kilimo ili kuweza kujenga viwanda vikubwa kutokana na mitaji ya wazawa na wageni kutoka SADC.
Aidha Waziri Mkuu, alisema kuwa Mkutano huo ni fursa kwa watanzania kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini ili kuweza kukuza sekta hiyo na kuwawezesha wageni kutoka nchi wanachama wa SADC kuja kuwekeza
“Watanzania tutumie pia fursa ya Mkutano huu wa SADC kutangaza vivutio vilivyoko nchini, ili tuweze kuleta watalii kuja kutalii hapa kwetu, banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lipo, lakini kila mtanzania popote alipo, kwa wakati wake, atumie muda wake kuwaeleza wageni ikiwezekana kuwapeleka kwenye maeneo ya utalii kwenda kutalii, aeleze kuhusu mbuga zetu kama vile Serengeti, Ngorongoro, Ruaha na Gombe, lakini pia Mlima kimanjaro, bonde la Olduvai Gorge na fukwe zetu nzuri ili wageni waweze kutembelea maeneo haya”, Kassim Majaliwa,Waziri Mkuu wa Tanzania.