Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaliwa: Hakuna Msamaha Kwa Wanaouibia Ushirika
Jul 01, 2017
Na Msemaji Mkuu

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma leo. Na Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitamsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhirifu wa mali na fedha za Ushirika nchini. Akiongea katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani iliyofanyika mkoani Dodoma Mh. Majaliwa alisema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwapeleka katika vyombo vya dola wezi wa mali na fedha za ushirika kwani wamekuwa wakirudisha nyuma maendeleo ya vyama hivyo. “Kwa Serikali hii ya awamu ya Tano tutachua hatua kali kwa wezi wa mali na fedha za ushirika na tunaendelea kufanya usafi wa wabadhilifu hadi tupate viongozi waadilifu,”. Amesema miongoni mwa changamoto zinazoukabili Ushirika nchini ni pamoja na wizi na ubadhilifu wa rasilimali za Ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wasiokuwa waaminifu. Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine ni baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika kutoheshimu miongozo ya vyama vyao na kujifanyia mambo kwa maslahi yao binafsi. Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake na kuweka mazingira rafiki ya kustawisha Ushirika nchini ili kutoa fursa ya Ushirika kushamiri na kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi yao. [caption id="attachment_4927" align="aligncenter" width="750"] Waziiri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli mbalimbali za korosho wakati alipotembelea banda la Ushirika wa Ruangwa, Nachingwea Liwale Cooperative Union (RUNALI) Limited katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma leo. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba[/caption] “Haikubaliki hata kidogo kuona sekta hii inayosadifu maisha ya Mwafrika haimnufaishi ipasavyo , hivyo naelekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ihakikishe kuwa vyama vya Ushirika vinaendeshwa kisayansi na kwa mujibu wa sheria,” amesema. Aidha amezielekeza Kamati za Ushauri za Mikoa na Wilaya nchini, ziingize agenda ya maendeleo ya ushirika kama moja ya agenda muhimu inayopaswa kujadiliwa na kuwekewa maazimio ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuwa na takwimu za vyama vya ushirika na wanachama wao. Hata hivyo Waziri Mkuu amezielekeza mamlaka zote zinazohusika na Ushirika nchini zijiwekee malengo yanayopimika ya namna ya kuboresha sekta hiyo. Katika hatua nyingine Mh. Majaliwa ameziagiza Wizara ya Kilimo na Uvuvi kuratibu masuala yote yanayohusu ushirika ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kufanyia mapitio kubaini elimu na ujuzi katika ngazi zote za ushirika kwa ajili ya kuwaandalia watumishi kozi za muda mfupi na kubainisha aina ya watumishi wanaohitajika kwenye sekta hiyo. Pia amewaagiza Maofisa Ushirika nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri uchaguzi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) na kuwaondoa wagombea wote waliowahi kuwa viongozi, ambao waliondolewa madarakani kutokana na ubadhilifu wa mali na fedha za Ushirika,

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi