Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakionyesha nakala za sera hiyo iliyozinduliwa na Waziri Mkuu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi, Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Dkt. Sophia Kongeli na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula nakala ya Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) baada ya kuzindua Sera hiyo kwenye Kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akiwasilisha taarifa katika Uzinduzi wa Sera ya Ubia ya NHC katika uzinduzi wa sera hiyo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2022.