Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua mradi wa maji wa Maghang Juu wilayani Mbulu akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Januari 24, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere na wa pili kulia ni Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Masay.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Masay (kulia) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kuzindua mradi wa maji wa Maghang Juu wilayani Mbulu akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Januari 24, 2022. Kushoto aliyebeba ndoo ya maji baada ya uzinduzi ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Maghang, Paulina Petro.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji wa Maghang Juu wilayani Mbulu akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Januari 24, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso.