Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaliwa Azindua Kiwanda cha Maziwa cha Mss Fresh Milk Mkoani Katavi
Dec 13, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua kiwanda cha maziwa cha MSS Fresh Milk katika jimbo la Nsimbi mkoani Katavi akiwa katika ziara ya mkoa huo, Disemba 13, 2022. Wa  tatu kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Salum Maliki, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi  na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu na kushoto ni Mbunge wa Nsimbo, Anna Lupembe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha MSS Fresh Milk cha Nsimbo, Salum Maliki (kushoto) kuhusu maziwa yanayozalishwa kiwandani hapo baada ya kuzindua kiwanda hicho, Disemba 13, 2022.  Kulia ni Mbunge wa Nsimbo, Anna Lupembe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua kiwanda cha maziwa cha MSS Fresh Milk katika jimbo la Nsimbo mkoani Katavi akiwa katika ziara ya mkoa huo, Disemba 13, 2022.  Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda, Salum Maliki, wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, kulia ni Naibu Waziri  Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, wa pili kulia ni Mbunge wa Nsimbo, Anna Lupembe. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavi,  Iddi Kimanta.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salum Maliki ambaye ni Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha MSS Fresh Milk cha Nsimbo Katavi kuhusu uzalishaji maziwa katika kiwanda hicho baada ya kukizindua akiwa katika ziara ya Mkoa wa Katavi Disemba 13, 2022. Kulia ni Mbunge wa Nsimbo, Anna Lupembe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Naibu Mawaziri, Wabunge na wafanyakazi wa kiwanda cha maziwa cha MSS Fresh Milk cha Nsimbo mkoani Katavi baada ya kuzindua kiwanda hicho, Disemba 13, 2022.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi