Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaliwa Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi Shule ya Sekondari Maji Moto
Dec 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Majimoto katika Halmashauri ya Mpimbwe akiwa katika ziara ya kikazi ya Mkoa wa Katavi Disemba 14, 2022. Kulia ni Mbunge wa Kavuu na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda, kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kavuu, Catherene Mashala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Majimoto katika Halmashauri ya Mpimbwe akiwa katika ziara ya Mkoa wa Katavi, Disemba 14, 2022. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, wa nne kushoto ni Mbunge wa Kavuu na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda, kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Majimoto katika Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, Disemba 14, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mbunge wa Kavuu, Geofrey Pinda ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Majimoto katika Halmashauri ya Mpimbwe akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Katavi Disemba 14, 2022. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavi, Iddi Kimanta, Diwani wa Kata ya Majimoto, Grace Udoba, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, Naibu Waziri  Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange na kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.
Muonekano wa majengo ya Shule ya Sekondari Majimoto ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake akiwa katika ziara ya Mkoa wa Katavi Disemba 14, 2022.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Majimoto katika Halmashauri ya Mpimbwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Majimoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Katavi, Disemba 14, 2022.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi