Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Majaliwa Atembelea Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati Katika Jiji La Dodoma
Dec 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39298" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uboreshaji wa Mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangali jijini Dodoma, wakati alipokagua Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika Jiji hilo, Desemba 29, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Gowin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption] [caption id="attachment_39299" align="aligncenter" width="937"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma, wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Watatu kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption] [caption id="attachment_39300" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji hilo, Desemba 29, 2018. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption] [caption id="attachment_39301" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi