Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihotubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Veta Jimbo la Ulyankulu wilayani Kaliua Mkoani Tabora leo August 11.2017, ambapo amewataka wananchi waliopewa uraia kuheshimu sheria za nchi vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa CUF Jimbo la Kaliua ,Magdalena Sakaya. Leo Agosti 11.2017,Waziri Mkuu yupo wilayani Kaliua kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Tabora.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mwamnange kilichopo Wilaya ya Kaliua leo Agosti 11 2017. Wananchi hao walisimamisha msafara wake ili kumuomba serekali iwasaidie kupata Umeme. Waziri Mkuu yupo Mkoani Tabora kukagua shughuli za maendeleo.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)