Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Ufunguzi wa Mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama Afrika
Feb 28, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria, Prof. Yemi Osibanjo (katikati) na Rais wa Mahakama hiyo, Imani Aboud (wa kwanza kushoto) wakisalimiana na Majaji, kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mhe. Majaliwa alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea nembo ya Mahakama ya Afrika kutoka kwa Rais wa Mahakama hiyo, Imani Aboud, alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo.
Baadhi ya washiriki wa ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria, Prof. Yemi Osibanjo (wa nne kushoto) na Rais wa Mahakama ya Afrika, Imani Aboud (wa tano kushoto) wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Wa pili kulia ni Waziri wa katiba na Sheria, George Simabachawene na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella. Wengine pichani ni Majaji wa Mahakama hiyo