Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Katika Mkutano wa Aqaba Process Nchini Jordan
Mar 25, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mfalme Abdulla II wa Jordan katika mkutano wa kujadili usalama kwenye eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika hususan nchini Msumbiji na maeneo jirani uliofanyika Machi 24, 2022 kwenye mji wa Aqaba nchini Jordan. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Mbarouk Nassor Mbarouk.