Majaliwa Ahutubia Katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Dawa za Kulevya Duniani
Jul 02, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es salaam, Julai 2, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Elizabeth Mramba (kushoto) kuhusu kitabu cha Riwaya kiitwacho Punje ya Tumaini katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye Viwanja Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam, Julai 2, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua kitabu cha Riwaya kiitwacho Punje ya Tumaini iliyotungwa na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Elizabeth Mramba (kushoto) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani Kwenye Viwanja Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam, Julai 2, 2022. Katikati ni Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya, kwenye viwanja viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam, Julai 2, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya (wa pili kushoto) wakati alipotembelea banda la Taasisi ya Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es salaam, Julai 2, 2022.