Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Magufuli Mwamba uliofanikiwa Vita ya Ufisadi na Rushwa
Jun 17, 2020
Na Msemaji Mkuu

Na Frank Mvungi, Dodoma

 Katika kupambana na adui rushwa, Taasisi yetu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeweza kufungua mashauri 2,256; ambapo mashauri 1,926 tayari yametolewa uamuzi, na Serikali imepata ushindi kwenye mashauri 1,013. Hayo ni sehemu ya maneno aliyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Magufuli wakati wa hotuba yake ya kuvunja Bunge la 11  June 16, 2020 Jijini Dodoma.

Dhamira hii ya Rais wetu mpendwa Dkt. Magufuli haina budi kuendelea kuungwa mkono na kila mtanzania ili kujenga taifa ambalo kila mwananchi ataendelea kunufaika na rasilimali zilizopo kama ilivyo sasa kwa kupiga vita rushwa.

Katika kipindi cha miaka mitano Rais Magufuli amebainisha kuwa  TAKUKURU imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 273.38, zikiwemo fedha walizokuwa wamedhulumiwa wakulima alieleza Rais Magufuli.

Mapambano haya yemewezesha wananchi kupata huduma bora za afya, elimu , miundombinu na maji kama alivyobainsha katika hotuba yake ya kuvunja Bunge la 11, mafanikio ni makubwa katika kila sekta ambapo kila mwananchi kwa sasa anatembea kifua mbele kwa mafanikio haya.

Aidha, Rais Magufuli anabainisha kuwa , TAKUKURU imetaifisha fedha taslim shilingi milioni 899, Dola za Marekani 1,191,651, EURO 4,301,399, nyumba 8 zenye thamani ya shilingi bilioni 11.6, magari matano yenye thamani ya shilingi milioni 126 pamoja na viwanja vitano (5).

Taasisi hii  imeweza kurejesha mali za Serikali zilizochukuliwa na watu binafsi ama taasisi kinyume cha sheria, zikiwemo nyumba na majengo 98 (ikiwemo Mbeya Hotel), mashamba 23, viwanja 298, kampuni 3, maghala 69.

Vile vile, kiasi cha fedha na mali zilizowekewa zuio kusubiria kukamilika kwa taratibu za kisheria za utaifishaji ni shilingi bilioni 52.7; Dola za Marekani milioni 55.8; Euro milioni 4.3, magari 75, nyumba 41; viwanja 47 na mashamba 13.

Hakika vyombo vya ulinzi na usalama vimefanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuiwezesha Serikali kushinda vita hii na kujenga misingi adhimu ya kutekeleza dhana hii.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi