[caption id="attachment_38104" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza jambo wakati akifungua mafunzo kwa Wahasibu kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini kutoka maeneo mbalimbali nchini (hawapo pichani) wanaohudhuria mafunzo ya Kielektroniki katika Ukusanyaji wa Mapato Serikalini (Goverment E- Payment Gateway – GePG) katika chuo cha Mazimbu Campus Solomn Maalangu mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo hayo.[/caption] Na Rhoda James – Morogoro
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Tume ya Madini kufuatilia madeni yote ya ada ya mwaka (Annual Rent) na kutoa muda kwa wahusika ili walipe ada hizo na endapo watashindwa kulipa katika muda watakaopewa, wapelekwe Mahakamani.
Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo Novemba 12, wakati akifungua mafunzo ya Wahasibu wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaohudhuria mafunzo hayo yanayohusu Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki katika Ukusanyaji wa Mapato (Goverment E- Payment Gateway – GePG). Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha Mazimbu Campus Solomn Mkoani Morogoro.
“Serikali inadai madeni mengi ya ada za mwaka, mfano kuna mtu moja ana leseni 103 na anaendela kuomba leseni nyingine lakini pia huyo mtu anadaiwa pesa nyingi za ada ya mwaka,” amesema Biteko.
[caption id="attachment_38103" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wahasibu (hawapo pichani) kutoka Wizara ya Madini nchini leo tarehe 12 Novemba, 2018[/caption]Naibu Waziri Biteko amesisitiza kuwa lengo la mfumo huo ni kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kupunguza mianya ya upotevu wa mapato kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi zote za Serikali.
Pia, Naibu Waziri Biteko ameongeza kuwa, ili kuleta tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, Mfumo wa GePG umeunganishwa na taasisi zinazotoa huduma za fedha kama vile Simu Benking za NMB na CRDB pamoja na Kampuni za Simu ambazo zinatoa huduma kupitia matawi, mawakala na mitandao ya simu lengo likiwa ni kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kutumia mfumo huo.
Akifafanua zaidi, Naibu Waziri Biteko amesema kuwa mafunzo hayo yapo kisheria na yanatokana na kifungu cha 44 cha Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 (The Finance Act, 2017) ambapo Wizara iliunganishwa rasmi kwenye mfumo huo mwezi Septemba, 2017.
[caption id="attachment_38100" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madani, Doto Biteko (kushoto) mara baada ya kusaini kitabu cha wangeni katika Ofisi ya Mratibu wa Chuo cha Mazimbu Campus Solomn Maalangu Dkt. Ibrahimu Mjema mkoani Morogoro.[/caption]Naibu Waziri Madini Biteko ameongeza kuwa, mnamo tarehe 4 Septemba, 2017 Serikali ilitoa Waraka wa Hazina Na. 3 kuhusu kutumia mfumo wa Serikali wa Kielektroniki katika Ukusanyaji wa Mapato lengo likiwa ni kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhusu kujengwa kwa mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko amewapongeza Wahasibu wote kwa kufanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 310 katika mwaka wa fedha 2018/19 na kueleza kuwa, mpaka kufikia tarehe 31 Oktoba, 2018 jumla ya maduhuli yenye thamani ya shilingi bilioni 111 yamekusanywa ambapo ni asilimia 36 ya lengo ambalo wizara iliwekewa kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19.
[caption id="attachment_38101" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Madani, Doto Biteko (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Uongozi kutoka Tume ya Madini na Chuo cha Mazimbu Campus Solomn Maalangu.[/caption] [caption id="attachment_38102" align="aligncenter" width="750"] Wahasimu kutoka Wizara ya Madini nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani).Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume, Prof. Shukrani Manya amesema kuwa, Mafunzo hayo ni muhimu kwa Tume ya Madini na kwamba yataleta fursa mbalimbali kama vile kujifunza na kuboresha utendaji wa wahasibu katika Tume ya Madini.
Mafunzo kama hayo yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo tarehe 28 hadi 31 Agosti, 2017. Kwa mwaka huu,mafunzo haya yameanza leo Novemba 12 na yanatarajia kukamilika tarehe 15 Novemba, 2018.