Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Madereva Bodaboda Wafurahishwa na Huduma za TRA
Jul 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33373" align="aligncenter" width="1000"] Wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa wameshika Namba za Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.[/caption]

Na Veronica Kazimoto - Dar es Salaam

Madereva wa Bodaboda ambao ni wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.

Madereva hao wapatao 20 wametembelea banda la TRA kwa ajili ya kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa lengo la kukatia leseni mara baada ya kumaliza mafunzo ya udereza wa pikipiki yaliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke kwa kushirikiana na umoja huo.

Akizungumza baada ya kusajiliwa madereva hao, Mwenyekiti wa umoja huo Said Kagomba amesema kuwa, amefurahishwa na huduma nzuri  waliyopatiwa na TRA ambapo wanachama wote wamesajiliwa na kupatiwa na TIN kwa muda mfupi.

[caption id="attachment_33374" align="aligncenter" width="750"] Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Helly Shindano akimhudumia dereva wa pikipiki katika banda la TRA wakati wa maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.[/caption] [caption id="attachment_33376" align="aligncenter" width="1000"]  Wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakisubiri kupatiwa huduma ya usajili na kupewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.[/caption]

"Mimi kama Kiongozi wa Umoja huu nimefurahia sana huduma tuliyopata hapa TRA, kwanza tumepokelewa vizuri na kisha tumehudumiwa haraka na kila mwananchama amepatiwa cheti chake cha TIN na sasa tunaendelea na hatua nyingine ya kwenda kukata leseni," alisema Kagomba.

Naye mmoja wa Madereva hao Ramadhan Mwilombwa ametoa wito kwa vijana kujiunga katika vyama mbalimbali kwa kuwa kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo, TIN na leseni kwa urahisi kwa sababu viongozi wa vyama husika wanajua sheria na taratibu mbalimbali.

"Ninaomba vijana wenzangu wajiunge na vyama hivi kwa sababu palipo na wengi hakiharibiki kitu. Mimi binafsi mpaka sasa nimepata faida nyingi za kujiunga na Umoja huu, kwanza nimepata mafunzo ya udereva na kujua vizuri sheria za barabarani, pili nimefahamiana na vijana wenzangu ambao nilikuwa siwafahamu hivyo nimeongeza marafiki, tatu nimefanikiwa kusajiliwa na TRA na kupata TIN na mwisho kiongozi wetu ametuambia tunakwenda kukata leseni," alifafanua Mwilombwa.

[caption id="attachment_33377" align="aligncenter" width="1000"] Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Jackline Lutare akisikiliza kero za mteja katika banda la TRA wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.   (Picha Zote na Benedict Liwenga)[/caption]

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa huduma mbalimbali katika Maonyesho ya Sabasaba.  Miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na kusajili walipakodi, kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, kutoa bili na kulipa Kodi ya Majengo.

Huduma nyingine ni kuelezea haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mashine za Kielektroniki za kutolea Risti (EFDs), kuelezea mwenendo wa makusanyo ya mapato ya Serikali, na kupokea maoni, malalamiko, mrejesho pamoja na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi