[caption id="attachment_47632" align="aligncenter" width="750"] Katibu mkuu , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa wadau wa lishe Jijini Dodoma Oktoba 4,2019 kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama.[/caption]
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Maafisa lishe nchini wametakiwa kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia lishe bora ili kuondoa changamoto ya utapiamlo na udumavu katika jamii.
Akizungumza wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa wadau wa lishe uliofanyika Jijini Dodoma Oktoba 4, 2019 kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi Waziri mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama, Katibu mkuu Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia Sera Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko amesema kuwa maafisa lishe wanapaswa kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau kuhusu umuhimu wa lishe bora.
“ Kipaumbele lazima kiwekwe katika makundi maalum kama wazee, watoto, akinamama wanajawazito na wale wanaonyonyesha ili kufanikisha azma ya Serikali kuondoa Changamoto ya utapiamlo na udumavu hapa nchini”; Alisisitiza Bi. Mwaluko.
Akifafanua amesema kuwa Serikali inasisitiza matumizi ya sanaa, vyombo vya habari na viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge katika kuelimisha umma kuhusu athari za utapimlo na udumavu hapa nchini.
[caption id="attachment_47633" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wake Katibu mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (Afya) Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa maazimio ya kikao hicho yanapaswa kutoa majawabu yatakayowezesha kuondokana na utapiamlo na udumavu hapa nchini.
Aliongeza kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi ya kufanya kazi na wadau katika kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu katika maeneo yote nchini ili kujenga jamii yenye afya bora.
Aidha, Dkt. Chaula aliwataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mapambano dhidi ya utapiamlo na udumavu hapa nchini ili kujenga jamii yenye afya bora hasa wakati huu Taifa linapojenga uchumi wa Viwanda na kutekeleza azma ya kuleta ustawi kwa wananchi.
Kikao kazi cha wadau wa lishe kimefanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma kikiwashirikisha wadau wa maendeleo, Maafisa lishe, Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Makatibu wakuu, Wabunge na Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali.
[caption id="attachment_47634" align="aligncenter" width="750"](Picha zote na Frank Mvungi)