Maafisa JWTZ Watembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Italia
Feb 04, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira pamoja na Col. Abdallah Khalfan wametembelea Ubalozi wa Tanzania Jijini Roma, Italia.
Wakiwa Ubalozini walipokelewa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia masuala ya ushirikiano. Maafisa hao walikuwepo nchini Italia kwa shughuli za kikazi.
Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira na Col. Abdallah Khalfan
Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira, Col. Abdallah Khalfan pamoja na baadhi ya watumishi wa Ubalozi