Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maafisa Habari Watakiwa Kuwa na Mawasiliano ya Kimkakati
Jul 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda akisisitiza jambo kwa Mwakililishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua hali itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma katika mkoa huo.[/caption]  

[caption id="attachment_33908" align="aligncenter" width="726"] Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Afisa Mipango Mji Bi. Mariam Kimolo wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo hivi karibuni.[/caption]

Frank Mvungi- MAELEZO

Maafisa Habari Katika Mkoa wa Mtwara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.

Akizungumza na Ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini  (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO uliomtembelea ofisini kwake , Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Alfred Luanda amesema kuwa jukumu la Maafisa Habari ni kuhakikisha kuwa masiliano kati ya Serikali na wananchi yanakuwa yakimkakati  na yanayoendana na kasi ya Serikali katika kuwahudumia wananchi.

“ Baadhi ya  Maafisa  Habari wanajiweka nyuma na kusahau kuwa wanalo jukumu kubwa la kuuhabarisha umma kuhusu miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao hasa kwenye Mikoa na Halmashauri” Alisisitiza Luanda

[caption id="attachment_33906" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bw. Omari Kipanga (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo hivi karibuni[/caption]

Akifafanua amesema kuwa umuhimu wa Afisa habari unatokana na namna anavyotekeleza majukumu yake  kwa weledi hasa katika suala la mawasiliano ya kimkakati.

Aidha,  alipongeza kazi zinazofanywa na Idara ya Habari na chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.

Kwa upande wake muwakilishi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo amesema kuwa kila Afisa Habari ana jukumu la kuisemea Serikali katika Mkoa au Halmashauri ili kuwapa wananchi fursa ya kuelewa mikakati ya na miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao na kuachana na kasumba ya kufanya kazi kwa mazoea.

[caption id="attachment_33903" align="aligncenter" width="900"] Afisa Habari wa Mkoa wa Mtwara Bw. Evaristi Masuha akisisitiza jambo kwa Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo hivi karibuni[/caption]

Naye Kiongozi wa ujumbe huo Bi. Gaudensia Simwanza amesema kuwa kuna haja kwa maafisa habari kupanua wigo wa utoaji wa taarifa za miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Aliongeza kuwa Lengo la chama cha maafisa habari na mawasiliano Serikalini ni kuwajengea uwezo katika kuisemea Serikali.

Ziara ya ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katika Mkoa wa Mtwara , Lindi na Ruvuma inalenga kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya ujumbe huo Maafisa Habari, na Viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa Halmashuri za Mikoa hiyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi