Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maafisa Habari Waaswa Kuongeza Kasi Kutangaza Mafanikio ya Serikali
Jun 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_44734" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi Sarah Kibonde akisisitiza umuhimu wa maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kutumia mbinu za kisasa katika kutangaza mafanikio ya Serikali , hayo yamejiri June 25, 2019 Jijini Dodoma wakati wa ziara ya ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO walipotembelea Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa lengo la kujionea utendaji wa Kitengo Cha mawasiliano Serikalini cha Tume hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa Umma.[/caption]

Na Frank Mvungi-  Dodoma

Kada ya Mawasiliano Serikalini imetajwa kuwa chachu ya kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano .

Akizungumza wakati wa ziara yakuwatembelea na kuona utendaji wa maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wa Mashirika na Taasisi zilizopo Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano  (TAGCO) Bi Sarah Kibonde  amesema kuwa  kuna umuhimu mkubwa kwa maafisa hao kutumia mbinu za kisasa kutangaza mafanikio ya Serikali.

“Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini   wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanatangaza mafanikio ya  Serikali ya Awamu ya Tano hasa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi hivyo tunawakumbusha wajibu huu  wa msingi ” Alisisitiza Bi Kibonde

[caption id="attachment_44735" align="aligncenter" width="750"] Naibu Msajili wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde akisisitiza jambo kwa ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO walipotembelea Tume hiyo wakati wa ziara yakutembelea Taasisi na Mashirika ya Umma yaliyopo Jijini Dodoma ili kujionea utendaji kazi wa vitengo vya Mawasiliano Serikalini vya Taasisi hizo.[/caption]

Akifafanua Bi Kibonde amesema  kuwa kwa sasa Serikali imewekeza katika miradi mingi ya maendeleo katika sekta zote zinazolenga kuleta ustawi wa wananchi na jukumu la kuitangza ni la kada hiyo.

Kwa upande wake muwakilishi wa  Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO katika ziara hiyo  Bw. Casmir Ndambalilo amesema kuwa Idara hiyo imejipanga na iko tayari kuendelea kuwajengea uwezo maafisa habari wote pale wanapohitaji ili kuwaongezea ujuzi zaidi.

Pia aliahidi kuwa Idara hiyo itaendelea kuhakikisha kuwa Maafisa hao wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na hasa katika kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano.

[caption id="attachment_44733" align="aligncenter" width="750"] Naibu Msajili wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde akisisitiza jambo kwa ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari –MAELEZO walipotembelea Tume hiyo leo Jijini Dodoma.[/caption] Ziara ya kutembelea Vitengo vya Mawasilaino Serikalini imefanyika katika taasisi za Serikali na Mashirika yaliyopo Dodoma kwa siku tano ikilenga kuona utendaji wa vitengo hivyo hasa katika kutekeleza jukumu la kuisemea Serikali kwa kutangaza mafanikio yake. [caption id="attachment_44736" align="aligncenter" width="750"] .Ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO ukiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Mhandisi Dkt Everest Makene(katikati) na watendaji wengine wa Taasisi hiyo June 25, 2019 wakati wa ziara yakufuatilia utendaji wa kitengo cha mawasiliano Serikalini katika Taasisi hiyo ili kujionea utendaji wake.[/caption] [caption id="attachment_44737" align="aligncenter" width="750"] Afisa Habari wa Jiji la Dodoma Bw. Denis Gondwe akisisitiza jambo kwa ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO walipotembelea Ofisi za Jiji la Dodoma leo kwa lengo la kuona utendaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Jiji hilo ikiwa ni sehemu ya juhudi zakuhimiza utoaji wa taarifa za miradi ya maendeleo kwa wananchi.[/caption] [caption id="attachment_44738" align="aligncenter" width="750"] Ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO ukiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Baltazar Ngowi leo Jijini Dodoma wakati wa ziara yakutembelea Kitengo cha mawasiliano Serikalini cha Jiji hilo ili kujionea utendaji wake.[/caption] [caption id="attachment_44739" align="aligncenter" width="750"] Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi Sarah Kibonde akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Baltazar Ngowi  Jijini Dodoma wakati wa ziara ya ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO kutembelea Kitengo cha mawasiliano Serikalini cha Jiji hilo ili kujionea utendaji wake.[/caption] [caption id="attachment_44740" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo kwa Naibu Msajili wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde wakati wa ziara ya ujumbe wa Idara hiyo na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) leo Jijini Dodoma.[/caption]

(Picha zote na  Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi