Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Maafisa Habari Kuweni Vinara Katika Kutangaza Habari za Serikali
Dec 03, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_49561" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipowasili katika viwanja vya Hazina kwa ajili ya kufungua awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma.[/caption]

Na Anitha Jonas & Shamimu Nyaki - WHUSM

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka Maafisa Habari nchini kuwa vinara katika kutangaza shughuli mbalimbali za serikali  ikiwemo miradi inayotekelezwa.

Mhe.Shonza ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya awamu ya pili ya Maafisa Habari nchini yanayofanyika kwa siku tano yenye lengo la kuwajengea uwezo.

[caption id="attachment_49563" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma.[/caption]

‘Katika kutangaza habari za serikali kwa umma kila Afisa Habari ni lazima kutumia vyanzo vyote kusambaza habari ikiwemo mitandao ya kijamii kwa sababu inasambaza habari kwa haraka zaidi na kufikia watu wengi,’alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi huo Naibu Waziri Shonza alisisitiza kuwa kwasasa waandishi wa habari  wanatakiwa kuwa na elimu kulingana na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kwani tasnia hii inatakiwa kuondokana na makanjanja.

Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amesisitiza kuwa Maafisa Habari wanapaswa kuandika na kutangaza habari za kimkakati zinazotekelezwa na serikali ili wananchi wafahamu maendeleo yanayofanywa na serikali.

[caption id="attachment_49564" align="aligncenter" width="985"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi awamu ya pili mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma..[/caption] [caption id="attachment_49565" align="aligncenter" width="1000"] Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi akitoa salaam za TAGCO mbele ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi awamau ya pili mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma.[/caption]

"Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kutangaza shughuli mbalimbali za serikali lakini wapo baadhi hawafanyi vizuri na ndiyo maana tumeona tuwape mafunzo haya ili kurekebishana  katika utendaji,"alisema Dkt.Abbasi.

Naye Katibu wa Chama cha Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Abdul Njaidi amesihi Maafisa hao kuzingatia elimu watakayoipata katika mafunzo hayo ili waweze kutangaza vizuri utekelezaji wa Serikali katika maeneo yao.

Pamoja na hayo mmoja wa Maafisa Habari  Bibi.Nuru Mfaume kutoka  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda alitoa shukrani zake kwa Msemaji Mkuu wa Serikali na uongozi wa TAGCO kwa mafunzo hayo ambayo yatawaongezea ujuzi.

[caption id="attachment_49566" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi nakala ya Jarida Maalum la Nchi Yetu Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza mara baada ya ufunguzi rasmi wa awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma. Jarida hilo ni toleo maalum linaloelezea mafanikio ya ndani ya Miaka Minne tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.Kulia ni Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi.[/caption] [caption id="attachment_49567" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akionyesha nakala ya Jarida Maalum la Nchi Yetu alilokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mara baada ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi,mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma. Jarida hilo ni toleo maalum linaloelezea mafanikio ya ndani ya Miaka Minne tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.Kulia ni Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi.[/caption] [caption id="attachment_49568" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_49569" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini mara baada ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo hayo leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi na Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi.[/caption] [caption id="attachment_49570" align="aligncenter" width="768"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akisindikizwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mara baada ya kufungua awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi,mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma. (Picha na Idara ya Habari –MAELEZO)[/caption]

"Kweli kabisa mafunzo haya yametusaidia kujitathimini utendaji wetu na kugundua makosa yetu na baada ya hapa hakika kutakuwa na mabadiliko katika utendaji ikiwemo uandishi wa habari zetu"alisema Bibi.Nuru.

Mafunzo hayo yanahudhuriwa na Maafisa Habari mia moja kutoka Wizara,Taasisi,Mashirika,Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara ambapo mada mbalimbali zitatolewa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi