[caption id="attachment_21302" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari na wakazi wa eneo la Tande kwa Mtogole wakati wa ziara ya waziri huyo ya kuzindua operesheni ya miezi miwili ya kusafisha mito nchi nzima.[/caption]
Na:Paschal Dotto
SERIKALI imewataka Wananchi kuzingatia usafi kuwa kusafisha mitaro na kuzibua maji yaliyopo katika mito ili kuepukana na adha ya mafuriko inayosababishwa kuwepo na taka ngumu zinazozuia utiririkaji wa maji kwa urahisi.
Akizungumuza katika uzinduzi wa Operesheni ‘Tudhibiti Uchafuzi wa Mazingira Tusalimike’ Jijini Dar es Salaam, itakayoanza nchini kote tarehe Novemba Mosi 1 hadi Desemba 30, mwaka huu, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola alisema ili jamii ibaki salama katika mazingira yao ni wajibu wao kuzingatia dhana ya usafi.
[caption id="attachment_21303" align="aligncenter" width="750"]“Uzalishaji wa taka ngumu ambao tumekuwa tukiufanya umesababisha kuziba mifereji ya maji, mitaro, na mito matokeo yake maji yametafuta mahali pakupita yakakosa na kuvamia makazi ya watu na ndiyo maana ya mafuriko huku Manzese Mtogole”, alisema Mhe. Lugola.
Aliongeza kuwa kupitia athari za mafuriko ya maji katika eneo hilo la kwa Mtogole, Wananchi wanapaswa kujifunza kuwa athari ya kutokufanya usafi na kuondoa taka ngumu na jinsi zinavyoweza kuleta athari katika makazi.
[caption id="attachment_21304" align="aligncenter" width="750"]Aidha Naibu Waziri huyo alitoa wito kwa wananchi kupitia Viongozi wa ngazi za mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi ya kuwaelimisha wananchi na kutoa vitendea kazi ikiwemo magari ya kuzolea taka.
“Halmashauri zote za Majiji, Manispaa na Miji pamoja zihakikishe zinawashirikisha Watanzania kwa asilimia 100 katika oparesheni Novemba Mosi kwa kuzibua mitaro, mifereji na mito karibu na makazi yao”,alisisitiza Mhe. Lugola.
Naibu Waziri Lugola pia alitoa onyo kwa watendaji wa halmashauri watakaokwepa kushiriki katika operesheni hiyo na kuwaasa kutoa msaada wa hali na mali utaohitaji kutoka kwa wananchi ili kuhakikisha kuwa inabaki Tanzania salama.