Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

LAPF Yajizatiti Kuwezesha Wajasiriamali Wadogo
Jul 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_5053" align="aligncenter" width="750"] Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara leo Jijini Dar es Salaam[/caption]

Frank Mvungi

Wajasiriamali wadogo wametakiwa kutumia fursa ya kuwepo kwaFao la Jiongeze scheme linalotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF ili waweze kukuza mitaji yao na hivyo kuchochea dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya Habari Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo Bw. James Mlowe amesema dhamira ya mfuko huo ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanakuwa na mazingira wezeshi kupitia fao hilo.

“Dhamira yetu ni kuona wajasiriamali hapa nchini wanashiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ndio sababu tumekuwa tukiboresha mafao tunayotoa mwaka hadi mwaka hali iliyochangia mwaka huu Mfuko wetu kuibuka washindi wa kwanza katika kundi la Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Taasisi za Bima zaidi ya 20” Alisisitiza Mlowe

Akifafanua Mlowe amesema kuwa kiwango cha uchangiaji kinaanzia shilingi 1000 hadi milioni moja kwa siku kutegemeana  na kiwango cha kipato cha mchangiaji na kupitia fao hilo mchangiajia naweza kujitoa na kutumia mafao yake kuendeleza biashara yake au huduma anayotoa.

Aliongeza kuwa maonesho ya       sabasaba ni fursa kwa mfuko huo kukutana na wananchi na wadau wake hali inayosaidia Mfuko huo kutoa elimu kwa umma na kusajili wajasiriamali wadogo pamoja na wachangiaji wengine ambao wameonesha kuvutiwa na mafao yanayotolewa na mfuko huo.

“Ofisi zetu katika maonesho ya sabasaba mwaka huu tunatoa huduma zote ambazo zinapatikana katika Ofisi zetu zote zilizopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini na dhamira yetu ni kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa bila kujali kundi analotoka mteja” Alisisiti za Mlowe

Mafao yanayotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF  ni pamoja na Fao la Uzazi, Fao la jiongeze Scheme, Fao la Elimu na fao la kuwawezesha waajiriwa wapya mara wanapoajiriwa iliwaweze kujikimu.

Mfuko wa Pensheni wa LAPF umeibuka mshindi wa jumla kati ya mifuko ya hifadhi za jamii hapa nchini na Taasisi zinazotoa huduma za bima hapa nchini zaidi ya 20 ambapo mifuko ya Hifadhi za Jamii nitakribani 7 ambayo imeshiriki katika maonesho hayo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi